Makala
KUENENDA KWA ROHO
| Makala
SHALOM MWANA WA MUNGU:
Mara kadhaa watu wengi sana wamejikuta wanaangukia katika mazingira ya dhambi bila kujitambua wala kuelewa nini kilichotokea mpaka wakaanguka,
Huenda wewe unayesoma ujumbe huu ndiyo mlengwa wa tatizo hili,na umekuwa ukitamani sana kuchomoka hapo kwa akili zako na umeshindwa mpaka umekata tamaa kabisa.
Na kwa bahati mbaya sana hata kama ukianguka kwa kujua au kutokujua adhabu iko palepale na Mungu hajatofautisha kabisa…
Hilo tatizo linazuilika kiroho, Unapomkaribisha Roho mtakatifu akuongoze kwenye maisha yako ya kila siku.
Ukisoma kitabu cha Wagalatia 5:16-26
Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.
Endelea kufuatilia zaidi haya mafundisho kupitia ukurasa wetu wa Youtube Channel ya SIRI ZA BIBLIA, Website ya www.sirizabiblia.com Na unaweza kujiunga nasi kwenye group la mafundisho na maombi kwa njia ya Whatssap kama bado hauja join kwa kutuma majina yako kwenda namba +255 758 708804 popote ulipo ulimwenguni.
Pastor Innocent Mashauri
Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA
Maarifa ya kiMungu
+255 758 708804
SADAKA